Stamina2
comments
capture-20140310-205906
comments
http://djchokamusic.com/wp-content/uploads/2014/07/Linah1.jpg
comments
Miaka michache iliyopita rapper Drake na Chris Brown walikua ni maadui wasiopikika chungu kimoja kutokana na penzi la mtoto Rihanna ambaye amewahi kuwa mpenzi wa kila mmoja wao.
dre
Picha mpya inayowaonesha Drake na Chris Brown wakiwa studio ni kiashirio tosha cha kumalizika kwa beef yao iliyopelekea ugomvi uliotokea kwenye club moja mwaka 2012.
Kwa mujibu wa mtandao wa Necolebithie, kuna shabiki mmoja aliyekuwa eneo la studio hiyo Los Angeles, na kupost kila kilichokuwa kikiendelea baada ya nyota hao kuwasili hapo studio.
-Ok this is huge. Drake just drove into Chris Brown’s studio. Chris Brown, Drake and Tyga are together right now. OMG
-I’m loving life right now Chris Brown, Karrueche,
-Drake, Tyga etc. the food, drinks and ice are arriving now! Hell yeahhh we want a collab
-Listening to some awesome tunes right now @Drake @chrisbrown @Tyga
-Sun’s coming up and @chrisbrown @karrueche @Drake @tyga are still in the studio love this
-Chris Brown, Drake & Karrueche just walked out of the studio together, said goodbyes, Drake left, then Chris left in his viper w/ Karrueche


Mara ya mwisho kwa Chris Brown na Drake kushirikiana kwenye wimbo ni katika ‘Dueces’. comments
Mama mzazi wa star anayeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa kwa sasa kupitia muziki, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz jana (July 11) alipata nafasi ya kuzungumza na Watanzania kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, mambo mbalimbali yanayomhusu mwanaye.
diamond na mama
Haya ni baadhi ya maswali ambayo aliulizwa na watangazaji wa kipindi hicho, pamoja na majibu aliyoyatoa:

Kuhusu tuhuma za Diamond kujihusisha na ushirikina katika muziki wake:
“Hiyo si kweli na wala hana ushirikina, si unajua tena mtu ukiwa juu kila mtu atakusingizia anachowaza yeye ili apate sifa ajulikane…Havijatokea watu uzushi tu wanapenda sasa ushirikina wa nini , kama mtu upo juu upo juu kama upo chini upo chini, nay eye sasa hivi ni nafasi yake kama sio nafasai yake atashuka walikuwepo wangapi, alikuwepo Mr Nice alikuwepo juu, lakini zamu yake imefika imeshuka imekuja zamu ya Nasib wacha awe juu itakapofika yake kushuka atashuka”.

Na hii tabia ya mara (msichana) huyu mara huyu wewe ukiwa kama mama kwako huo unaipokea vipi?
“ Siipokei vizuri laikini sasa nitafanya nini nay eye star, wengine wanajitongozesha bila kutongozwa..mi mwenyewe hapa kutwa napigiwa simu mpaka nazima, wananipigia simu wanafikiria Nasib wanajitongozesha mpaka nawatumia meseji mbona mnajitongozesha, hii sio namba ya Nasib hii namba katoa ya biashara ya Tshirt 0716186318 sio namba ya Diamond, namba yake mama yake.sitaki usumbufu..wananitumia mapicha ya uchi , mapicha ya nini sasa ni ustarabu gani huo”

Yanasemwa mengi kuhusu mahusiano ya Diamond na Wema mara tunasikia kuna Penny…lakini katika habari za pembeni za wadaku watu wanasema mama yake Diamond anampenda zaidi Penny, hilo liukweli mama?
“Mimi sina ninayemchukia, kwasababu mimi mama na mimi nina mtoto wangu wa kiume, akiniletea mkwe siwezi kumkataa, yeye ni wa kiume na lijal, je angekuwa nanii (shoga) mi ningeletewa mwanamke? Nisingeletewa, sasa watu wanavyosema hivyo sijui nampenda nani si kweli mi yeyote anayekuja mi nampenda siwezi kumchukia mtu wote binadamu wenzangu”.

Kwasababu umeishi na Penny na Wema kwa muda wote, Penny ni msichana wa aina gani na wema ni msichana wa aina gani?
Mi navyoona wote sawa kwasababu wananionesha mapenzi wote wananipenda, siwezi kusema nimchukie Penny mtoto wa watu siwezi kumchukia, alikuwa ananionesha upendo unajua tu tena ni ibilisi mwenyewe manake mambo yao mi siwezi kuingilia, lakini wote naona wananipenda.

Wewe unavyoona mama Diamond muda wa kuoa umefika ama bado?
“Umefika lakini mwenyewe bado hajaamua, namwambia lakini mwenyewe anakwambia bado mama, nahitaji mkwe nahitaji mjukuusi unajua tena, nataka mtoto kumwona bado nanguvu zangu nikishakuwa kizeesiwezi kumlea”

Unatamani Diamond aoe mwanamke wa aina gani?
Sasa hayo ni maamuzi yake siwezi kumpangia mwanamke ila napenda mtu awe na nidhamu , anajali familia yake na familia ya kiumeni, sio mwanamke mapepe anajijali mwenyewe hamna, mtu unapokuja sehemu penda familia ukipenda …. upende na…. habari ndio hiyo. comments
Muimbaji wa label ya Choclate City ya Nigeria, Mkenya Victoria Kimani alikuwepo nchini kwa kwaajili ya utengenezwaji wa video ya single yake ‘Prokoto’, aliyowashirikisha Diamond na Ommy Dimpoz ambayo audio tayari ilishatoka.
kimani
Video hiyo ilishutiwa jana (July 11) jijini Dar es salaam na kuongozwa na director Kevin Bosco wa Kenya aliyeongoza video ya AY ‘Asante’.
Diamond aliyewasili nchini Juzi uziku (July 10) akitokea Marekani, pamoja na Ommy Dimpoz ambao wote wameshirikishwa kwenye wimbo huo wameshiriki pia katika video.
prokoto shoot1
Kupitia ukurasa wa Instagram wa WCB_Wasafi ya Diamond walipost picha ya Dimpoz, Diamond na Victoria wakiwa kwenye moja ya locations.
prokoto shoot2
comments
Miezi michache iliyopita Roma aliahidi kubadilisha mfumo aliokuwa akiutumia wa kutoa wimbo mmoja kwa mwaka, na kusema sasa ataanza utaratibu wa kutoa wimbo zaidi ya mmoja kwa mwaka ili kukata kiu ya mashabiki wake. Ahadi hiyo aliitoa wakati anaachia single yake ya ‘KKK’ mwezi March mwaka huu.
Roma
Rapper huyo kutoka Tanga anaelekea kutimiza ahadi yake sababu tayari ameanza kutease single yake mpya ‘Ukombozi’ aliyowashirikisha Mwana FA, Mwasiti na Jay Moe, iukiwa ni miezi minne toka single iliyopita.
Kupitia ukurasa wake wa facebook na Instagram Roma ametease mistari michache kutoka kwenye single hiyo kwa kuandika:
RHYMES OF MAGIC ATTRACTION
Loading……

Aliumbwa Adam sijamaanisha Mchomvu/
Akaja Eva aliyetoka kwenye ubavu/
Leo kina Hawa tunawatoa chini ya kitovu/
Na sisi ndiyo kina Adam basi tuwapeni mashavu/
Ouuuuu!!!
R.O.M.A. ft. Mwana F.A/ Jay Moe/ Mwasiti
“UKOMBOZI” ” UKOMBOZI” ” UKOMBOZI”
Yoh partnaz ar u ready 4 dis…!!?
Huh!!?…. comments
10448978_1440928429511842_1735172974_n
Mkali wa muziki kutoka pande za manzese aka raisi wa mazense, Madee anatarajia kushusha homa nyingine ya jiji hivi karibuni, Madee aliweza ku-make headlines east africa nzima kupitia nyimbo yake ya “pombe yangu”, nyimbo iliyosumbua sana media za hapa jijini, na kabla hata wadau wa muziki na mashabiki wake hawajaanza kumsahau na kabla hata nyimbo yake hiyo ikiwa bado inafanya vizuri kwenye media mbali mbali hapa bongo, anatarajia kushusha kali nyingine mapema hivi karibuni, ngoma hiyo itakayokwenda kwa jina la “Ni sheeda” kazi iliyosimamiwa na producer Marco Chali. comments
Golikipa wa Marekani, Tim Howard jana amevunja rekodi ya dunia kwa kuokoa mipira 15 ya hatari golini kwakuwa kitu kama hicho kilifanyika kwa mara ya kwanza 1966.
howard2
Mlinda mlango wa Peru, Ramon Quiroga alikuwa anashikilia rekodi nyingine kwa kuokoa mipira 13 wakati timu yake ikicheza na Uholanzi mwaka 1978. Pamoja na jitihada hizo, Marekani ilitolewa na Ubelgiji kwa kufungwa mabao 2-1. Kutokana na hatua hiyo, Howard amegeuka kuwa shujaa wa Marekani na jina lake limetrend kwenye Twitter. comments
Huenda ilikuwa ni sababu watu walitegemea kuwaona Beyonce na Jay Z ama tumbuizo lililosubiriwa kwa hamu kutoka Chris Brown baada ya kutoka jela, lakini vyovyote ilivyokuwa, tuzo za BET zilizofanyika Jumapili iliyopita ziliangaliwa na watu milioni 7.9.
nicki-minaj_1
Idadi hiyo ni kuwa zaidi tangu mwaka 2009 – mwaka ambao BET ilifanya maadhimisho ya Michael Jackson. Tuzo za BET ziliwazidi kwa mbali wapinzani wake, MTV Awards, ambao walipata watazamaji milioni 3.2.
Pia tuzo hizo ziliongelewa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko hata Billboard Music Awards, Golden Globes, People’s Choice Awards, fainali za NBA ama mechi ya kombe la dunia kati ya Ureno na Marekani. comments
Rapper Shetta amedai kuwa baada ya kutoka kwa video yake mpya ya Kerewa tayari ameshaanza kupata deal za pesa ambapo DSTV wameshaonyesha nia ya kufanya kazi na msanii huyo.
kerewa
Akizungumza na 225 ya XXL ndani ya Clouds FM, Shetta amesema kuwa tayari wapo kwenye mazungumzo na no na DSTV na hivi karibuni kila kitu kitakuwa wazi.
“Wakati Diamond ananiambia ‘weka hela Shetta usiogope kuweka hela kutangaza muziki wako kuwa tofauti na wanamuziki wengine, fanya muziki wako kufika mbali’, akimaanisha soko la Afrika nikaona kama ananitania hivi, almost alikuwa ananiambia kama milioni 20 hivi ukiitoa ile hela ambayo Godfather ninamlipa, nikaona mbona ni pesa nyingi sana. Lakini nimejaribu kudhubutu, hiki unachokiona ni king’amuzi cha DSTV ni kama fursa ambayo nimekutana nayo ni deal ambayo ikiwa rasmi zaidi watu watagundua nini ambacho kimetokea, lakini mpaka hapa tulipofikia ni kama nusu yake au robo tatu yake. Godfather aliniconnect na watu wa DSTV, tukafanya makubalianao na makaratasi yapo. Video yangu imepata rotation kubwa sana, katika station zote ambazo zinaonekana DSTV, na wamenifollow kwenye akaunti zangu, wananitangazia vitu vyangu kwenye akaunti zao, kwahiyo hiyo ni deal kwa upande wangu. Thanks to Diamond, thanks to Tale na watu wote ambao wamenisupport. Kwahiyo sijutii kwa pesa niliyoweka,” alisema. comments
Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa kupanda jukwaa moja na rapper Nicki Minaj, Macklemore and Ryan Lewis, J Cole na Kid Ink kwenye tamasha kubwa zaidi kuwahi kutokea barani Afrika, la Tribeone Dinokeng’ litakalofanyika Tshwane, nchini Afrika Kusini mwezi September mwaka huu.
10378148_776635619026578_5357518240846368181_n
Wasanii wengine wa Afrika watakaotumbuiza ni pamoja na Jaguar, Redsan, Nameless na Xtatic wa Kenya, Wizkid wa Nigeria, Fally Ipupa wa Congo, Maurice Kirya, Keko, Naava Grey wa Uganda pamoja na rappers wa Afrika Kusini, Khuli Chana na AKA.
bendi
Tamasha la ‘TribeOne Dinokeng’ limeandaliwa na ROCKSTAR4000 na Sony Music Entertainment na litafanyika 26-28 September. comments
Mshindi wa tuzo ya BET 2014 ‘Best International Act: Africa’ Davido pamoja na aliyekuwa nominee mwenzake katika kipengele alicho shinda, Tiwa Savage jana (June 30) walipata nafasi ya kuhojiwa na Revolt TV ya Marekani, inayomilikiwa na rapper na mfanya biashara Sean “Diddy” Combs.
Davido Revolt
Davido
Msanii mwingine aliyepata shavu hilo ni rapper wa Chocolate City, Ice Prince pia kutoka Nigeria.
Tiwa Revolt
Tiwa Savage
Ice Revolt
Ice Prince
Fursa kama hizi kwa wasanii wa Afrika kupata nafasi ya kutambuliwa na vituo vikubwa vya kimataifa ni hatua muhimu na ya mafanikio kwa wasanii wa Kiafrika. comments
Beyonce Knowles amekamata nafasi ya kwanza katika orodha ya mwaka huu ya watu mia moja maarufu duniani kwa mujibu wa Forbes.
bey
Mama Blue Ivy amemwondoa Oprah aliyekamata nafasi hiyo kwenye orodha ya mwaka jana, na kutupwa katika nafasi ya nne katika orodha ya mwaka huu.
dre2
Dr Dre ni kati ya walioingia Top 5 na amekamata nafasi ya 3, huku Ellen DeGeneres ameshika nafasi ya 5.
Jay Z ameshika nafasi ya sita huku star wa ‘Diamonds’ Rihanna ameshika nafasi ya nane.
Jarida la Forbes imeandaa orodha hiyo kwa kuangalia umaarufu pamoja na uwezo wa kipesa, baada ya kufuatilia kipato walichoingiza kwa shughuli zinazohusiana na burudani kwa kipindi cha kuanzia June 1, 2013 hadi June 1, 2014.
Kwa mwaka huu nguvu ya umaarufu ilitazamwa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii, pamoja na mara ngapi watu hao walitajwa katika magazeti, radio na TV.
Forbes 2014 Celebrity Top 10
1.Beyonce Knowles, $115 million
2.LeBron James, $72 million
3.Dr. Dre, $620 million
4.Oprah Winfrey, $82 million
5.Ellen DeGeneres, $70 million
6.Jay-Z, $60 million
7.Floyd Mayweather, Jr., $105 million
8.Rihanna, $48 million
9.Katy Perry, $40 million
10.Robert Downey Jr., $75 million comments
Copyright © 2014 BABA JONII